• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Vijana Afrika: Rwanda yatangaza majina ya wawakilishi wake watakaokwenda Algeria

  (GMT+08:00) 2018-06-12 09:06:30

  Shirikisho la mchezo wa riadha nchini Rwanda RAF limetangaza majina 18 ya awali ya wachezaji watakaoingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya vijana ya Afrika yatakayofanyika nchini Algeria Julai 18 hadi Julai 28.

  Katika Majina hayo kuna wanariadha chipukizi 9 wanaume na chipukizi 9 wanawake na wamegawanywa katika makundi matatu ya kiushindani, mbio za mita 3000, mita 1,500 na mita 800.

  Kwa mujibu wa RAF Wanariadha hao sasa wanatarajiwa kuanza kambi ya mazoezi kwa ajili ya maandalizi wiki hii.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako