• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lakaribisha usitishaji vita wa muda Afghanistan

  (GMT+08:00) 2018-06-12 09:07:47

  Baraza la usalama la Umoja wa mataifa limekaribisha uamuzi wa serikali ya Afghanistan uliotangazwa wiki iliyopita wa kusitisha mapambano kwa muda na kundi la Taliban, kwa ajili ya kumalizika kwa mwezi mtakatifu wa Ramadhani na kukaribisha sikukuu ya Eid al-Fitr. Baraza hilo pia limepongeza uamuzi wa Taliban kusitisha vita kwa siku tatu, na kuwataka waitikie kikamilifu wito wa serikali wa kusitisha mapambano. Wajumbe wa baraza hilo wamelitaka kundi la Taliban kukubali mwaliko wa serikali wa kushiriki kwenye mazungumzo ya amani bila masharti au matishio yoyote, kwa lengo la kufikia ufumbuzi wa mwisho wa mgogoro kati ya pande hizo mbili na kutimiza amani ya kudumu nchini humo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako