Baraza la usalama la Umoja wa mataifa limepitisha uamuzi wa kurefusha vikwazo vya silaha dhidi ya Libya kwa mwaka mmoja zaidi. Kupitia mswada wa azimio Nambari 2420 ulioandaliwa na Uingereza, baraza hilo limeamua kurefusha muda wa vikwazo hivyo vilivyowekwa mwezi Juni mwaka jana. Kwa mujibu wa azimio hilo, nchi wanachama wa Umoja wa mataifa zimepewa mamlaka kukagua meli kwenye bahari kuu zinazitia shaka zikitoka au kuelekea Libya, na kukamata na kushughulikia silaha zinazogunduliwa kwenye meli hizo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |