• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marekani yaweka vikwazo vipya dhidi ya mashirika na watu binafsi wa Russia kutokana na usalama mtandaoni

  (GMT+08:00) 2018-06-12 09:08:40

  Wizara ya fedha ya Marekani imetangaza kuwa itaweka vikwazo vipya dhidi ya mashirika matano na watu watatu wa Russia, kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya hujuma kwenye mtandao wa Internet. Taarifa iliyotolewa na waziri wa fedha wa Marekani Bw. Steven Mnuchin inasema mashirika na watu hao wamechangia moja kwa moja kuboreshwa kwa uwezo wa Russia kwenye mtandao, kushirikiana na Idara ya usalama ya Russia FSB, na hivyo kuhujumu usalama wa Marekani na washirika wake. Wizara hiyo pia imetaja warussia wengine sita watakaowekewa vikwazo kwa tuhuma za kujihusisha na mambo ya Libya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako