• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Timu ya Buzz Pirates yashinda mzunguko wa kwanza

  (GMT+08:00) 2018-06-12 09:19:08

  Timu ya Buzz Pirates imefanikiwa kushinda kwenye mechi ya fainali ya mkutano wa kwanza wa michuano ya kitaifa ya mchezo Raga kwa wachezaji saba kwa mwaka huu nchini Uganda.

  Pirates ilishinda hatua hiyo ya kwanza kwa kuifunga timu ya Betway Cobs kwa alama 21-7 katika mchezo uliokuwa mgumu.

  Kabla ya kufuzu fainali, Pirates walifanikiwa kushinda mechi zote za awali, 38-0 dhidi ya Stallions, 29-0 dhidi ya Buffaloes, 22-0 dhidi ya Hippos na kwenye mechi ya nusu fainali waliwashinda Hima Cement kwa 35-10.

  Pirates sasa wanamaliza raundi hii iliyofanyika mjini Kyandondo wakiwa washindi, sasa wanajiandaa na raundi ya pili itakayofanyika wiki chache zijazo mjini Kabale.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako