• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Patrick Vieira atangazwa kuwa kocha mpya wa klabu ya Nice

  (GMT+08:00) 2018-06-12 09:20:12

  Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa na klabu ya Arsenal Patrick Vieira ametangazwa kuwa kocha mpya wa klabu ya Nice inayoshiriki ligi ya nchini Ufaransa kwa mkataba wa miaka mitatu na akichukua nafasi ya Lucien Favre aliyehamia Borussia Dortmund.

  Kutokana na heshima aliyojizolea pamoja na uzoefu aliopata kwenye kazi ya ukufunzi wa soka, viongozi wa Nice wamesema, Vieira anafaa kwa kazi hiyo.

  Vieira alianza kazi ya ukufunzi katika kikosi cha akiba cha Manchester city na baadaye akateuliwa kuwa kocha mkuu wa New York City inayoshiriki ligi kuu nchini Marekani, huku mwenyewe akiwaambia waandishi wa habari kuwa anafurahia kurejea Ufaransa baada ya miaka 20 ya kutumikia nje ya taifa hilo kwenye majukumu mbalimbali ya kisoka.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako