• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wasisitiza udharura wa kuchangia pesa kutimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu

    (GMT+08:00) 2018-06-12 09:24:04

    Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Bw. Miroslav Lajcak amesisitiza udharura wa kuchangia pesa kwa ajili ya kutimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu SDGs.

    Bw. Lajcak amesema Malengo hayo yanahitaji uwekezaji wa kimataifa wa dola za kimarekani trilioni 5 hadi 7 kila mwaka, kiasi ambacho ni asilimia 7 hadi 10 tu ya pato la dunia au asilimia 25 hadi 40 ya uwekezaji wa kimataifa kila mwaka. Hata hivyo amesema fedha zipo lakini hazipatikani kwa urahisi, na inabidi mbinu na mifumo mipya vijaribiwe kutoka kukusanya fedha kwa njia ya mseto, hadi kuhamasisha raslimali za ndani ya nchi.

    Ameomba juhudi zifanyike kushirikisha sekta binafsi katika kuchangia pesa ili kutimiza Malengo hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako