• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wasema hali ya Darfur imeboreshwa

    (GMT+08:00) 2018-06-12 09:24:38

    Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia operesheni za kulinda amani Bw. Jean-Pierre Lacroix amesema hali katika jimbo la Darfur nchini Sudan imeboreshwa, na mapigano kati ya serikali na makundi ya waasi yanaendelea katika sehemu za milimani katika eneo la Jebel Marra tu.

    Akitoa ripoti kwa Baraza la Usalama juu ya Kikosi cha Kulinda amani cha Pamoja cha Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa huko Darfur UNAMID, Bw. Lacroix amesema kutokana na mabadiliko hayo, shughuli za kulinda amani zinapaswa kurekebishwa ili kuhudumia vizuri watu wa jimbo hilo. Ameongeza kuwa wakati umefika kwa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kuweka mpango wa kujenga amani na maendeleo, badala ya kulinda amani.

    Amekumbusha kuwa UNAMID inatekeleza majukumu yake ya mwaka wa mwisho, ambapo vituo 11 vya vikosi vimefungwa na ulinzi wa amani utaendelea katika eneo la Jebel Marra peke yake, huku ujenzi wa amani ukianza katika sehemu nyingine za jimbo la Darfur.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako