• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za Afrika Mashariki zaiangalia Hong Kong kama lango la soko la nyama la Asia kusini mashariki

    (GMT+08:00) 2018-06-12 09:28:25

    Nchi za Afrika Mashariki chini ya Shirika la maendeleo la kiserikali la nchi za Afrika Mashariki IGAD, zimesema zinapenda kuingia kwenye soko la nyama na wanyama hai la Asia Kusini mashariki kupitia Hong Kong.

    Nchi za IGAD ambazo mara nyingi huuza nyama na wanyama hai kwa nchi za Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, zimesema soko la Hong Kong linaweza kupunguza changamoto zilizopo kwenye biashara hiyo na nchi za mashariki ya kati na Afrika Kaskazini.

    Licha ya ukaribu na nchi za IGAD, nchi za mashariki ya kati na Afrika Kaskazini zina uwezo wa kukidhi asilimia 50 na asilimia 10 mtawalia ya mahitaji ya soko kwa nchi za IGAD.

    Hong Kong inaweza kuwa lango kwenye soko la miji mbalimbali yenye idadi ya watu milioni 66.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako