• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mashirika mawili yazindua mradi wa kutoa fursa za kupata fedha kwa vijana na wakimbizi Kenya

  (GMT+08:00) 2018-06-12 09:28:43

  Mashirika mawili ya kimataifa yamezindua mradi mpya utakaotoa fursa za kupata pesa kwa wakimbizi na vijana wa Kenya wanaoshi kwenye kambi ya Dadaab. Mradi huo wa kutoa ajira kwa wakimbizi na ujuzi kwa wakimbizi (RESI) umezinduliwa na Kituo cha Biashara cha kimataifa na Baraza la wakimbizi la Norway (NRC).

  Mradi huo utatumia motisha wa soko kuhimiza kujikimu endelevu kwa wakimbizi na watu wa jamii inayopokea wakimbizi.

  Mkuu wa baraza la wakimbizi la Norway Bw Andrea Bianchi amesema mpango huo utaliwezesha baraza hilo kufanya kazi kwa karibu zaidi na wadau wa maendeleo, ikiwa ni pamoja na serikali ya kaunti ya Garissa na kuwa na mpango wa jumla kwenye kazi zake na kusaidia watu kujikimu.

  Kambi ya wakimbizi ya Dadaab ilifunguliwa mwaka 1991, na sasa ina wakimbizi laki 2.5 kutoka Somalia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako