• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Afrika Kusini yataka maoni ya umma kwenye mswada wa taifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa

    (GMT+08:00) 2018-06-12 09:29:01

    Wizara ya mambo ya mazingira ya Afrika Kusini imeutaka umma wa nchi hiyo kutoa maoni kwenye mswada unaoandaliwa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa.

    Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo inataka warsha za wadau wa majimbo ziwawezeshe wadau wote na wengine wanaopenda kutoa maoni yao kwenye warsha zitakazoendeshwa katika nchi nzima.

    Lengo la mswada huo ni kujenga mwitikio wenye ufanisi katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, na kuhakikisha kunakuwa na mpito wa muda mrefu na wa haki, kuelekea uwezo wa kuvumilia mabadiliko ya hali ya hewa, na kuwa na uchumi na jamii inayotoa uchafuzi kidogo.

    Mswada huo unaitaka serikali kuu, serikali za majimbo na serikali za mitaa kuratibu juhudi zao ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako