• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Morocco na Nigeria zaahidi kuweka mfano wa Ushirikiano wa Kusini na Kusini

  (GMT+08:00) 2018-06-12 09:42:43

  Mfalme wa Morocco Mohammed wa Sita na rais Muhammadu Buhari wa Nigeria wamesisitiza tena dhamira yao ya kuweka mfano wa Ushirikiano wa Kusini na Kusini.

  Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa kufuatia ziara ya rais Buhari nchini Morocco, viongozi wa nchi hizo mbili wamepongeza uhusiano uliopo kati ya Morocco na Nigeria tangu Mfalme wa Morocco Mohammed wa Sita alipofanya ziara nchini Nigeria mwaka 2016.

  Viongozi hao wamepongeza mafanikio makubwa yaliyopatikana kwenye ushirikiano wa sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kilimo, uzalishaji wa mbolea, miundombinu ya nishati na uchimbaji madini.

  Viongozi hao pia wamesisitiza dhamira yao ya kuimarisha uratibu kati ya nchi zao kwenye mashirika ya kikanda na ya kimataifa, ikiwemo Umoja wa Afrika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako