• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zimbabwe na China zasaini makubaliano kuhusu kuanzisha kiwanda cha chuma cha pua

    (GMT+08:00) 2018-06-12 09:58:34

    Zimbabwe na China zimesaini makubaliano yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 1 kwa ajili ya kuanzisha kiwanda cha chuma cha pua ambacho kitazalisha tani milioni 2 za chuma cha pua kwa mwaka.

    Makubaliano hayo yalisainiwa mwanzoni mwa mkutano wa siku nne wa Baraza la biashara kati ya Zimbabwe na China. Katibu mkuu wa kamati ya Chama cha Kikomunisti cha China ya mkoa wa Zhejiang Bw. Che Jun ameongoza ujumbe wa China kushiriki kwenye mkutano huo.

    Bw. Che amesema ujumbe huo unatafuta fursa za biashara na uwekezaji nchini Zimbabwe, ili kuisaidia nchi hiyo kukuza uchumi. Vilevile amesema mkoa wa Zhejiang una nia ya kuwekeza nchini Zimbabwe, ili nchi hiyo iweze kunufaika na ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako