• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wawili wa kundi la waasi Ethiopia warudi nyumbani baada ya kufanya mazungumzo na serikali

    (GMT+08:00) 2018-06-12 10:12:13

    Viongozi wawili wa kundi la waasi wa Ethiopia wamerudi nyumbani baada ya kufanya mazungumzo na waziri mkuu wa nchi hiyo Bw. Abiy Ahmed.

    Shirika la habari la Ethiopia ENA limeripoti kuwa Bw. Yonatan Dubissa na Bw. Abebe Geresu waliokuwa wanafanya operesheni zao kutoka nchini Eritrea, baada ya kujiunga na kundi haramu la Oromo Liberation Front OLF, wamerudi nyumbani baada ya kufanya mazungumzo na waziri mkuu.

    Ripoti imesema Bw. Dubissa na Bw. Geresu ambao walikuwa upande wa serikali kabla ya kujiunga na kundi la waasi, walianza mazungumzo na waziri mkuu mpya wa Ethiopia baada ya kushuhudia mabadiliko ya kisiasa nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako