• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kim na Trump wakutana kihistoria

  (GMT+08:00) 2018-06-12 10:26:13

  Kiongozi mkuu wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un na rais Donald Trump wa Marekani wamefanya mkutano  katika hoteli ya Capella, nchini Singapore. Mkutano ulianza saa tatu asubuhi kwa saa za huko.

  Hii ni mara ya kwanza katika historia kwa viongozi wa Korea Kaskazini na Marekani walioko madarakani kukutana ana kwa ana.

  Kabla ya mkutano wao uliohudhuriwa pia na maofisa wanaoambatana nao, viongozi hao walishikana mikono mbele ya wanahabari na bendera za nchi zao, huku Rais Trump akisema "huu ni mwanzo mpya", na kufanya mkutano mfupi wa faragha, ambao Rais Trump amesema umetatua tatizo moja kubwa.

  Viongozi hao wawili wanatarajiwa kufanya majadiliano ya kina kuhusu kuanzisha uhusiano mpya kati ya nchi zao, kujenga utaratibu wa kudumu na imara wa kulinda amani kwenye Peninsula ya Korea, kuondoa silaha za nyuklia kwenye Peninsula hiyo na masuala mengine wanayofuatilia kwa pamoja.

  Saa chache kabla ya mkutano wao, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amepongeza viongozi hao wawili kutokana na juhudi zao za kutatua maswala kwa njia za kidiplomasia. Pia ametoa shukrani kwa watu wote ambao wamefanya juhudi za kuandaa mazingira kwa ajili ya mkutano huo. Amesisitiza kuwa amani na uondoaji wa silaha za nyuklia unaoweza kuthibitishwa katika Peninsula ya Koreaļ¼Œbado ni lengo wazi na la pamoja, na utimizaji wake unahitaji ushirikiano, kurudi nyuma na dhamira ya pamoja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako