• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Majaji wa Afrika wakutana Tanzania kwenye mkutano kuhusu usawa wa kijinsia

  (GMT+08:00) 2018-06-12 13:01:04

  Mkutano kuhusu Jinsia na Mahakama barani Afrika umefanyika nchini Tanzania ukiwa na lengo la kushughulikia vikwazo vya kisheria kwa wanawake katika nchi za Afrika.

  Makamu wa Rais wa Tanzania Bibi Samia Suluhu amesema katika mkutano huo ulioandaliwa na Mahakama ya Tanzania na Benki ya Dunia kuwa viwango vya umaskini barani Afrika vinazuia wanawake kupata huduma za mahakama.

  Jaji Mkuu wa Tanzania Bw. Ibrahim Juma amesema kupata haki kwa usawa ni sehemu muhimu ya maendeleo ya binadamu, na kuondoa umaskini ni nyenzo muhimu ya mkakati wenye msingi wa haki za binadamu katika kuhimiza maendeleo ya kiuchumi.

  Ofisa mwandamizi wa Benki Kuu ya Dunia Bw. Sandie Okoro amesema ili kuhakikisha uaminifu na ufanisi wa mfumo wa mahakama, mahakama zinatakiwa kuzingatia watu wa rangi na jinsia tofauti.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako