• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: 'Tuko tayari kuwekeza Tanzania' yasema Uturuki.

    (GMT+08:00) 2018-06-12 18:26:26
    Serikali ya Uturuki imesema mazingira ya biashara na uwekezaji nchini, ni mazuri na kuahidi kuendeleza diplomasia ya uchumi na Tanzania.

    Hayo yalisemwa na Balozi wa Uturuki nchini, Ali Davutoglu na kufafanua kuwa yanaruhusu ushindani wenye usawa sokoni jambo ambalo ni zuri.

    Aliyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wa futari iliyoandaliwa na Shirika la Ndege la Uturuki (Turkish Airlines) kwa ajili ya wateja, mawakala wa tiketi, maofisa wa ubalozi na wadau wengine. Katika miaka 18 iliyopita, alisema biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Uturuki umeimarika na utaendelea kushamiri zaidi.

    Naye meneja masoko wa Turkish Airlines, Taylan Saylam alisema mfungo wa Ramadhan ni wakati mahsusi kwa watu kukaa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako