• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Uagizaji wa chakula cha nje wafikia shilingi bilioni 68

  (GMT+08:00) 2018-06-12 18:26:44
  Bei ya uagizaji wa chakula na Kenya kutoka mataifa ya nje imefikia shilingi bilioni 68.63 pesa za Kenya, kwa miezi minne iliyopita. Kwenye takwimu zilizokusanywa na Benki kuu ya Kenya, zinaonyesha kuwa bei hii ilipanda kwa asilimia 30.10 katika ya mwezi Januari hadi Aprili, ikilinganishwa na shilingi bilioni 52.75 kwa kiwango sawa na hicho mwaka uliopita. Hii ina maana kwamba kutegemea kwa chakula cha msaada na Kenya kunazidi kuongezeka sana licha ya hali nzuri ya hewa ya ukulima ambayo imekuwa ikishuhudiwa. Utegemezi wa chakula cha nje umeongezeka zaidi ya mara nne unusu kwa mwaongo mmoja. Kati ya mwezi Januari na Aprili mwaka wa 2008, Kenya ilitumia shilingi bilioni 15.09 kwa ununuzi wa chakula kutoka mataifa mengine. Baadhi ya vyakula vinayoagizwa na Kenya ni kama vile mahindi, ngano, mchele na sukari.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako