• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Marekani na kiongozi wa Korea Kaskazini wasaini makubaliano ya kina

    (GMT+08:00) 2018-06-12 19:02:25

    Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un na rais Donald Trump wa Marekani wamesaini makubaliano ya kina leo mchana nchini Singapore.

    Katika hafla ya kusaini makubaliano hayo, rais Trump amesema waraka huo ni muhimu, na wa makubaliano ya kina. Naye kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ameuita waraka huo kuwa ni wa kihistoria, akisema pande hizo mbili zitaachana na mambo yaliyopita, na dunia itashuhudia mabadiliko makubwa.

    Katika taarifa yao ya pamoja, rais Trump ameahidi kutoa uhakikisho wa usalama kwa Korea Kaskazini, huku kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akirejea ahadi yake ya kuondoa silaha za nyuklia kwenye peninsula ya Korea. Viongozi hao wamekubaliana kuanzisha uhusiano mpya kati ya nchi hizo kuendana na matakwa ya watu wa nchi hizo kwa ajili ya amani na ustawi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako