• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Jumuiya ya kimataifa yatumai SCO itaingia katika kipindi kipya

  (GMT+08:00) 2018-06-12 19:45:17

  Mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai (SCO) uliofanyika Qingdao, China, umemalizika hivi karibuni.

  Rais Xi Jinping wa China alitoa hotuba kuhusu maendeleo ya SCO, uhusiano kati ya jumuiya hiyo na mashirika mengine ya kimataifa, na usimamizi wa dunia. Naibu mkurugenzi wa Benki ya Dunia anayeshughulikia mambo ya Asia ya mashariki na Pasifiki Bw. Victoria Kwakwa amesema, hotuba ya rais Xi inaunganisha uongozi wa taifa na maendeleo ya uchumi pamoja na maisha ya watu, na kwamba mazungumzo ndio njia sahihi ya kutimiza kunufaishana.

  Mjumbe kudumu wa Russia katika sekretariat ya SCO Bw. Dmitry Lukiansev amesema, inapaswa kutimiza lengo la pamoja na kunufaishana kwa ajili ya wenzi wa ushirikiano, kwa sababu makubaliano na ushirikiano ni maelewano kati ya nchi mbalimbali za SCO na kanuni ya "moyo wa Shanghai".

  Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa bibi Amina J. Mohammed amesema, ushirikiano kati ya SCO na Umoja wa Mataifa katika miaka kadhaa iliyopita umefanyika juu ya msingi wa ushirikiano wa pande mbalimbali na maoni ya pamoja, na kuhimiza amani, usalama, na maendeleo ya uchumi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako