• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yapongeza mkutano kati ya viongozi wa Marekani na Korea Kaskazini kupata matokeo mazuri

  (GMT+08:00) 2018-06-12 19:59:15

  Wizara ya mambo ya nje ya China leo imetoa taarifa kuhusu mkutano wa viongozi wa Marekani na Korea Kaskazini nchini Singapore.

  Taarifa hiyo imesema, mkutano huo umefanyika na kupata matokeo mazuri, na ni maendeleo muhimu ya kuhimiza peninsula ya Korea kutokuwa na silaha za nyuklia na mchakato wa kutatua suala la peninsula ya Korea kwa njia ya kisiasa. China inapongeza matokeo hayo na kuziunga mkono, na kupongeza juhudi za pande mbalimbali kwa ajili ya mkutano huo.

  Taarifa hiyo imesisitiza kuwa, China inashikilia kutimiza peninsula ya Korea kutokuwa na silaha za nyuklia, kulinda amani na utulivu wa peninsula hiyo, kutatua suala hilo kwa mazungumzo, na kufanya juhudi kwa ajili ya masuala hayo. China inatumai na kuunga mkono utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa Marekani na Korea Kaskazini, kusukuma mbele mazungumzo ya baadaye na kuimarisha na kupanua zaidi mafanikio, ili utatuzi wa kisiasa wa suala la peninsula ya Korea kuwa mchakato endelevu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako