• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya yafanya mazungumzo na Uganda kuhusiana na wavuvi waliofungwa

  (GMT+08:00) 2018-06-13 09:35:17

  Mamlaka za Kenya zinafanya mazungumzo na Uganda kuhusu kuachiwa huru kwa wavuvi nane waliokamatwa kwenye ziwa Victoria kwa kosa la kuingia Uganda kinyume cha sheria.

  Naibu msemaji wa polisi wa Uganda Bw. Paul Onyango amesema wavuvi hao wa Kenya walikamatwa na maofisa wa Mamlaka ya Mapato ya Uganda kwa kosa la kuvua samaki kinyume cha sheria kwenye maji ya Uganda. Msemaji huyo amesema upande wa Kenya na Uganda wanafanya mazungumzo ili kuachiwa huru kwa wavuvi hao.

  Kenya na Uganda zimekuwa na mikwaruzano ya mara kwa mara kutokana na mambo ya uvuvi kwenye ziwa Victoria, hasa kwenye kisiwa kinachogombewa cha Migingo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako