• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rwanda yapanda daraja, sasa kutangaza njia mpya itakayotumika mwaka huu

  (GMT+08:00) 2018-06-13 09:40:44

  Shirikisho la mchezo wa mbio za Baiskeli nchini Rwanda FERWACY leo mchana linatarajiwa kutangaza barabara mpya zitakazounda mzunguko mzima wa mashindano ya kimataifa kwa mwaka huu ya nchini humo, mtandao wake ukitarajiwa kuwa mpya na wa daraja la juu kwa kuwa mabadiliko haya ni kwa mujibu wa kanuni zinazoongoza mchezo huo duniani.

  Mashindano haya ni awamu ya kumi tangu taifa hilo lianze kuandaa, na yanatarajiwa kuanza rasmi Agosti 5 na kumalizika Agosti 12, ikiwa ni tofauti na ratiba ya miaka iliyopita ambapo Rwanda ilikuwa inaandaa mashindano hayo mnamo mwezi Novemba.

  Kwa viwango vya dunia Rwanda sasa inakuwa nchi ya pili kwa barani Afrika kupanda daraja la viwango vya ubora wa mashindano kutoka 2.2 kwenda 2.1, kwani mpaka sasa ni taifa la Gabon pekee ndio lilikuwa na kiwango hicho.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako