• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wizara ya Michezo kuchunguza mgomo wa wachezaji kugoma

  (GMT+08:00) 2018-06-13 09:41:49

  Waziri wa michezo wa Kenya Rashid Echesa amesema wizara yake inaendelea na uchunguzi dhidi ya mgomo uliofanywa na timu ya taifa wa kutovaa jezi zenye nembo ya mdhamini kwenye mashindano ya kimataifa ya wachezaji saba (seven series) yaliyofanyika mjini Paris nchini Ufaransa.

  Waziri Echesa alisema kuwa, ni kweli wachezaji pamoja na benchi la ufundi wanadai shilingi milioni 4, lakini kwa mujibu wa makubaliano ya kikao kuhusu suala hiyo kati ya serikali na timu, ilikuwa kwamba fedha hizo zilipwe mara tu baada ya mashindano ya Ufaransa.

  Lakini cha ajabu, wakiwa kwenye mashindano, timu haikutumia jezi zenye nembo ya mdhamini mkuu ambaye ni Brand Kenya katika mechi zote walizoshiriki, na sasa serikali inafanya uchunguzi ili kubaini waliohusika na kukiuka makubaliano ili hatua zichukuliwe.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako