• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Timu ya taifa yashinda nafasi ya pili kwenye mzunguko wa kwanza wa kufuzu

  (GMT+08:00) 2018-06-13 09:42:10

  Timu ya taifa ya Uganda, ya mchezo wa mpira wa kikapu (Silverbacks) imeshinda nafasi ya pili katika kundi la raundi ya kwanza ya makundi ya kwanza mechi za kufuzu kombe la dunia mwaka 2019, ikiwa nyuma ya Nigeria inayoongoza kundi hilo, na mbele ya Mali na Rwanda ambazo licha ya kulingana nazo pointi imezidi kwa upande wa alama za ushindi.

  Katika raundi hiyo ya kwanza, Uganda imeshinda mechi moja tu kati ya tatu ilizocheza kwenye kundi hilo zilizofanyika nchini Mali.

  Raundi ya pili ya hatua ya makundi ya kwanza ya kufuzu inatarajiwa kufanyika kuanzia Juni 29 hadi Julai 1 mwaka huu nchini Nigeria, na kocha mkuu wa Uganda Mohamed Santur akitarajiwa kufanya mabadiliko kadhaa ya wachezaji kwenye kikosi chake.

  Ili kufuzu hatua ya pili ya makundi ya pili ya kufuzu, Uganda italazimika kushinda walau mechi moja kati ya tatu itakazocheza nchini Nigeria.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako