• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Azamc FC yamwajiri Mwambusi kuwa msaidizi wa kocha mkuu

  (GMT+08:00) 2018-06-13 09:43:59
  Klabu ya soka ya Azam FC ya Tanzania jana imeingia mkataba na Juma Mwambusi wa kuwa kocha msaidizi wa timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili.

  Juma Mwambusi ambaye ni kocha mzoefu sasa atakuwa msaidizi wa kocha mpya wa timu, Hans Van Pluijm ambaye hivi karibuni naye aliingia mkataba na klabu hiyo.

  Mwambusi na Pluijm wamewahi kufanya kazi pamoja wakiwa katika klabu ya Yanga misimu mwili ilyopita, kabla ya Pluijm kuhamia Singida United na Mwambusi kuamua kupumzika.

  Azam FC msimu uliopita haikuwa na mwenendo wa kuridhisha kwenye ligi hivyo mabadiliko haya ni maandalizi ya msimu ujao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako