• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Deontay Wilder wa Marekani akubali kupigana na Anthony Joshua

  (GMT+08:00) 2018-06-13 09:44:18

  Bingwa wa uzani mzito duniani Deontay Wilder amekubali kuzipiga dhidi ya Anthony Joshua nchini Uingereza.

  Raia huyo wa Marekani mwenye umri wa miaka 32 anashikilia taji la WBC na anataka pigano la kuunganisha mataji hayo na Anthony Joshua anayeshikilia mataji matatu ya WBA, IBF na bingwa wa WBO.

  Promota wa Joshua, Eddie Hearn amesema kuwa kweli amepokea jibu la Wilder la kukubali kupigana katika pambano lenye thamani ya dola za milioni 50 na anatarajia kutuma hati za kandarasi hiyo lakini hajui iwapo madai hayo ya Wilder yana ukweli wowote.

  Muda na mahali pa pambano vitathibitishwa baada ya hati hiyo kupitishwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako