• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya yasaini makubaliano na Singapore kumaliza kutozwa ushuru mara mbili

  (GMT+08:00) 2018-06-13 09:46:00

  Kenya imesaini makubaliano na Singapore kumaliza kutozwa ushuru mara mbili, na kuvutia uwekezaji kutoka nchi hiyo kwenye sekta muhimu ikiwemo usindikaji wa mazao ya kilimo na huduma za fedha. Waziri wa fedha na mipango wa Kenya Bw. Henry Rotich amesema kufutwa kwa ushuru wa mara mbili kutahimiza biashara kati ya nchi hizo mbili, na kubadilishana uzoefu na utaalamu unaohitajika katika kuendeleza uchumi. Kwa mujibu wa waziri huyo, thamani ya bidhaa za Kenya zilizouzwa nchini Singapore mwaka jana ambazo ni pamoja na chai, matunda na mboga, ilikuwa ni dola za kimarekani milioni 30, huku thamani ya bidhaa za Singapore zilizoingizwa Kenya mwaka huo ikifikia dola milioni 50.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako