• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania yapanga kuendeleza kilimo cha maua

  (GMT+08:00) 2018-06-13 10:02:27

  Naibu waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji wa Tanzania Bibi Stella Manyanya amesema, Tanzania inashughulikia mradi unaopangwa kukabiliana na changamoto zinazolikabili sekta ya kilimo cha maua, unaotoa mamilioni ya nafasi za ajira kwa watanzania.

  Bibi Manyanya amesema kwenye mkutano wa bunge unaoendelea mjini Dodoma, kuwa Tanzania imeamua kuwasaidia wakulima wa maua kuingia kwenye soko la ndani na la kimataifa kupitia mradi wa mfuko wa Umoja wa Mataifa SECO.

  Kwa mujibu wa mradi huo, Bibi Manyanya amesema Tanzania inashirikiana na serikali ya Switzerland kukusanya na kutangaza habari kuhusu soko kwa washiriki ikiwa ni pamoja na bei, wateja, na upatikanaji wa bidhaa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako