• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Naibu rais wa Afrika Kusini asema wagonjwa wote wa kifua kikuu nchini humo lazima watibiwe

  (GMT+08:00) 2018-06-13 10:09:35

  Naibu rais wa Afrika Kusini Bw. David Mabuza amesema wagonjwa wote wa kifua kikuu nchini Afrika Kusini ni lazima watibiwe ili kutokomeza ugonjwa huo kabla ya mwaka 2030 kulingana na lengo la maendeleo endelevu la Umoja wa Mataifa.

  Akihutubia mkutano wa tano wa ugonjwa wa kifua kikuu wa Afrika Kusini uliofanyika mjini Durban, Bw. Mabuza amesema Afrika Kusini imefanya juhudi kuwatambua wagonjwa wote wa kifua kikuu kama nchi nyingine zinavyofanya duniani.

  Mkutano huo umefanyika kwa lengo la kutoa mapendekezo ya kiutendaji na kuwatafuta wagonjwa wote wa kifua kikuu. Bw. Mabuza ameongeza kuwa mkutano huo pia umetoa nafasi ya kubadilishana uzoefu kuhusu njia ya kuimarisha mfumo wa afya na jamii.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako