• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Ufaransa atoa mwito kwa Iran kuheshimu wajibu wake kwa mujibu wa makubaliano ya nyuklia

  (GMT+08:00) 2018-06-13 10:16:29

  Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amerudia msimamo wake wa kufuata makubaliano ya nyuklia ya Iran na kuitaka Iran itekeleze wajibu wake bila kutetereka, licha ya Marekani kujitoa kwenye makubaliano hayo.

  Akizungumza na mwenzake wa Iran Hassan Rouhani kwa njia ya simu, rais Macron amekumbusha dhamira ya Ufaransa, Uingereza, Ujerumani, Russia na China ya kuendelea kutekeleza makubaliano haya kwa pande zote.

  Rais Hassan Rouhani amezitaka nchi za Ulaya zilizosaini makubaliano hayo kuchukua hatua zinazotekelezeka na za kivitendo kulinda maslahi ya Iran. Ameongeza kuwa haiwezekani kwa Iran kuendelea kuwepo kwenye makubaliano hayo, kama haitanufaika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako