• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini na China zasaini makubaliano ya maendeleo ya vyombo vya habari

    (GMT+08:00) 2018-06-13 10:17:24

    Sudan Kusini na China zimesaini makubaliano ya ushirikiano wa kiufundi yanayolenga kukarabati studio za vituo vya redio na televisheni vinavyomilikiwa na serikali kuwa za kisasa.

    Naibu katibu wa Wizara ya Habari na Matangazo ya Sudan Kusini Bw. Justin De Mayen amesema mradi huu utakaofadhiliwa na China unakadiriwa kugharimu dola za kimarekani milioni 15, na utasaidia kujenga studio mbili za kisasa na kujenga uwezo wa wanahabari wa Sudan Kusini kupitia mawasiliano ya vyombo vya habari. Ameishukuru China kutokana na uungaji mkono wake kwa maendeleo ya sekta ya habari nchini Sudan Kusini na kuongeza kuwa nchi hizo mbili zitaendelea kuimarisha uhusiano kwa ajili ya maslahi ya wananchi wao.

    Konsela wa uchumi na biashara wa ubalozi wa China nchini Sudan Kusini Bw. Cai Senmin amesema mradi huo utakaotekelezwa na wahandisi wa China utaanza hivi karibuni, na kuongeza kuwa China inapenda kufanya juhudi za kusaidia nchi hiyo kupata utulivu na maendeleo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako