• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wasema China inafanya kazi muhimu na chanya katika hali ya Peninsula ya Korea

    (GMT+08:00) 2018-06-13 10:19:36

    Umoja wa Mataifa umeipongeza China kutokana na kazi zake muhimu na chanya katika hali ya Peninsula ya Korea.

    Pia umesema katibu mkuu wa Umoja huo Antonio Guterres amepongeza kufanyika kwa mkutano wa kihistoria kati ya viongozi wa Marekani na Korea Kaskazini na kuutaja kuwa ni tukio muhimu.

    Msemaji wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric, amesema Bw. Guterres hajabadilisha msimamo wake katika kuondoa silaha za nyuklia katika Peninsula ya Korea, kuwa uondoaji wa silaha hizo unatakiwa kuwa kamili, wa kuthibitishika na kutorudia.

    Wakati huohuo, Shirika la Habari la Korea Kaskazini KCNA limeripoti kuwa kiongozi mkuu wa nchi hiyo Bw. Kim Jong Un amekubali mwaliko uliotolewa na rais Donald Trump kufanya ziara nchini Marekani, na rais Trump pia amekubali mwaliko wa Bw. Kim kutembelea Korea Kaskazini katika wakati mwafaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako