• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watu 75 wafariki kwa kipindupindu nchini Kenya tangu Januari

  (GMT+08:00) 2018-06-13 10:22:35

  Mkurugenzi wa idara ya huduma za matibabu ya wizara ya afya ya Kenya Bw. Jackson Kioko amethibitisha kuwa watu 75 wamefariki kutokana na kipindupindu katika miezi mitano iliyopita.

  Bw. Kioko ameongeza kuwa watu 4,954 walithibitishwa kuambukizwa ugonjwa huo tangu uliporipotiwa kwa mara ya kwanza, na wilaya 19 zimethibitishwa kukumbwa na ugonjwa huo, na tisa kati ya hizo zilifanikiwa kuudhibiti, na nyingine 10 zinaendelea kuripoti wagonjwa wapya kila siku.

  Maabara ya Taifa ya Afya ya Umma imetoa huduma za msaada wa vifaa vya upimaji na sampuli za majaribio kupelekwa katika maabara ya taifa, kutoa taarifa kuhusu tahadhari na kuimarisha usimamizi kwa walioambukizwa

  .

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako