• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • AU yapongeza juhudi za Sudan kupatanisha pande hasimu Sudan Kusini

  (GMT+08:00) 2018-06-13 10:28:09

  Umoja wa Afrika umekaribisha pendekezo la Sudan kuwa mwenyeji wa mkutano kati ya Rais Kiir na Bw. Machar, na kusema unakaribisha hatua yoyote inayoweza kutimiza amani ya Sudan Kusini.

  Balozi wa Sudan nchini Sudan Kusini Bw. Adil Ibrahim Mustafa, amesema juhudi za upatanishi za Sudan katika mazungumzo kati ya viongozi husika wa pande zinazopingana zitamaliza migongano na kuleta amani nchini humo.

  Bw. Mustafa amesema huko Juba kuwa mazungumzo yaliyopangwa kati ya rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Bw. Riek Machar, yanatarajiwa kuanza Juni 18.

  Balozi huyo pia amesema, mazungumzo hayo yatatilia maanani masuala yenye mvutano kati ya pande hizo zinazopingana na kuhudhuriwa na waziri mkuu mpya wa Ethiopia Bw. Abiye Ahmed na viongozi wengine wa nchi za Jumuiya ya IGAD.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako