• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya yazindua sera mpya ya usimamizi wa ardhi ili kukabiliana na bei za juu

  (GMT+08:00) 2018-06-13 16:03:22
  Naibu Rais wa Kenya William Ruto amesema bei ya ardhi jijini Nairobi iko juu kupita maelezo,hivyo ipo haja ya sekta hiyo kudhibitiwa.

  Akizungumza Jumanne katika ukumbi wa KICC, Nairobi wakati wa uzinduzi wa sera mpya ya usimamizi wa ardhi ya taifa, Bw Ruto alisema usimamizi mbaya wa ardhi ndio hufanya bei kuwa ya juu kupita kiasi mbali na kuibua changamoto zingine kama vile ueneaji wa mitaa ya mabanda na unyakuzi wa maeneo muhimu ya kutunza mazingira.

  Alisema katika baadhi ya maeneo Nairobi ambako bei ya ardhi ni kati ya Sh500 milioni na Sh600 milioni kwa ekari moja, ni kutokana na mipangilio mibaya na ukosefu wa mwongozo wa wazi kuhusu matumizi ya ardhi.

  Kulingana na Bw Ruto, sera hiyo iliyoandaliwa na Wizara ya Ardhi na Mipango ya Ujenzi itasaidia pia kukabiliana na uchipuzi wa mitaa ya mabanda na kudhibiti bei ya ardhi ambayo kulingana naye imekuwa ya juu kupita kiasi.

  Kati ya Sh17 bilioni zinazonuiwa kutumiwa kwa utekelezaji wa sera hiyo, imependekezwa Sh4 bilioni zitumiwe kurudisha hali halisi ya ardhi zilizo katika maeneo ya kuvutia mvua na za ufuoni.

  Waziri wa Ardhi Bi Farida Karoney, alisema sera hiyo itasaidia serikali kufanikisha malengo yake makuu ya maendeleo hasa katika uzalishaji wa chakula cha kutosheleza mahitaji ya wananchi na ujenzi wa nyumba bora za bei nafuu mijini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako