• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda-Serikali yajengwa viwanda vya Chai kwa gharama ya Sh9.bn

  (GMT+08:00) 2018-06-13 16:03:58
  Shirika la Maendeleo Uganda (UDC),ambalo ni shirika la uwekezaji la serikali,limeanzisha ujenzi wa viwanda viwili vya majani chai magharibi mwa Uganda vitakavyogharimu jumla ya Sh19.1bn.

  Chai imezingatiwa kama bidhaa inayopewa kipaumbele na ya kimkakati katika sekta ya kilimo,ambayo kulingana na Mkurugenzi Mtendaji wa UDC Bw Emmanuel Mutahunga,itachangia ukuaji katika usafirishaji wa bidhaa ya majani chai.

  Alisema serikali imetia saini mkataba wa ufadhili na kampuni ya majani chai ya Kigezi Highland Tea kununua,kusimika,na kuanzisha kiwanda cha uzalishaji kilo 450 kwa saa.

  Alisema kiwanda kingine kilichofaidika na mpango huu ni kile cha Kabale ambacho tayari ujenzi umekamilika na kimeanza kufanya kazi.

  Majani chai yote yanayosindikwa katika kiwanda cha Kabale husafirishwa katika soko la mnada wa chai mjini Mombasa huku kiwanda hicho kikisafirisha tani 25 kila wiki.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako