• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kilimo cha matunda na mboga chakadiriwa kuajiri watu milioni 2.4 Tanzania

  (GMT+08:00) 2018-06-13 16:04:15

  Kilimo cha matunda na mboga kinakadiriwa kuajiri watu milioni 2.4 nchini Tanzania,wengi wao wakiwa ni wanawake.

  Hayo yalibainishwa jana bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Viwanda,Biashara ,na Uwekezaji,Bi Stella Manyanya.

  Manyanya alisema serikali imekuwa ikiweka kipaumbele katika kutambua fursa za masoko ya matunda na mboga ndani na nje ya nchi.

  Alisema serikali kwa kushirikiana na Tanzania Horticulture Association (TAHA),imeandaa mafunzo kwa wakulima wa matunda na mboga kutoka mikoa ya Arusha,Kilimanjaro,Morogoro,Iringa,Njombe,Mbeya,na Zanzibar na inaendesha mafunzo ya kilimo bora cha bidhaa hizo ili kukidhi matakwa ya masoko ya ndani na nje ya nchi.

  Aidha alisema mafunzo hayo pia yatafanyika katika mikoa iliyobaki ili kuwasaidia wakulima wa nchi nzima kupata soko la ndani na nje ya nchi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako