• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kujenga utaratibu wa kurekebisha bima ya malipo ya uzeeni kati ya mikoa mbalimbali

    (GMT+08:00) 2018-06-13 17:50:55

    China itajenga utaratibu wa kurekebisha bima ya malipo ya uzeeni kati ya mikoa mbalimbali, ili kuhakikisha wazee wa sehemu tofauti wanapata bima wanayostahili kwa wakati.

    Baraza la serikali ya China limeamua kujenga mfuko wa kurekebisha bima ya malipo ya uzeeni, ili kurekebisha akiba ya mikoa mbalimbali kwa ajili ya kuhakikisha watu wa sehemu tofauti wanapata bima ya malipo ya uzeeni kwa wakati. Naibu waziri wa nguvu kazi na huduma za jamii wa China Bw. You Jun ameeleza sababu ya kujenga mfuko huo ni changamoto ya ukosefu wa uwiano kati ya mikoa, katika akiba ya bima ya malipo ya uzeeni. Amesema hivi sasa China imefanikiwa kuwapatia wachina wote walioko mijini na vijijini bima ya malipo ya uzeeni, na akiba ya jumla ya bima hiyo ni ya kutosha. Hata hivyo kutokana na ongezeko la wazee na mabadiliko ya hali ya ajira, baadhi ya mikoa inakabiliwa na upungufu wa akiba ya malipo ya bima ya uzeeni. Anasema,

    "Sehemu zilizoendelea zikiwemo Beijing, Guangdong zina akiba ya kutosha, wakati huo huo baadhi ya mikoa ikiwemo Liaoning na Heilongjiang ina pengo kati ya mapato na malipo ya bima ya uzeeni."

    Bw. You Jun amesema fedha za mfuko wa kurekebisha bima ya malipo ya uzeeni utakaoanzishwa na serikali kuu, zitatoka katika bima za mikoa mbalimbali, halafu fedha hizo zitarudishwa kwenye mfuko wa bima ya malipo ya uzeeni ya mikoa yenye upungufu. Anasema,

    "Mfuko wa kurekebisha bima ya malipo ya uzeeni utapata fedha kutoka bima ya malipo ya uzeeni kutoka mikoa mbalimbali. Watu bado hawajatoka michango ya kutosha. Madhumuni ya kujenga mfuko huo, ni kurekebisha bima kati ya mikoa."

    Utaratibu wa kurekebisha bima ya malipo ya uzeeni kati ya mikoa mbalimbali utatekelezwa kuanzia tarehe mosi Julai. China imeagiza kuwa fedha za mfuko wa kurekebisha bima ya malipo ya uzee haziwezi kutumiwa kwa matumizi mengine isipokuwa bima ya malipo ya uzeeni tu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako