• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wasema China imechukua nafasi kubwa katika suala la Peninsula ya Korea

    (GMT+08:00) 2018-06-13 19:36:59

    Msemaji wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema, China imechukua nafasi muhimu na chanya katika suala la Peninsula ya Korea.

    Hali ya peninsula hiyo imeingia kwenye historia mpya wakati jamii ya kimataifa ikisifia mkutano kati ya rais wa Marekani na kiongozi wa Korea Kaskazini.

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amepongeza mkutano huo na kusema ni hatua kubwa muhimu katika suala la Peninsula ya Korea. Guterres ameipongeza China kwa kuchukua nafasi muhimu katika kusuluhisha suala la Peninsula ya Korea mwezi April, siku chache baada ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un kufanya ziara nchini China, ikiwa ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa Korea Kaskazini kufanya ziara nje ya nchi tangu aingie madarakani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako