• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Jeshi la muungano linaloongozwa na Marekani lafanya mashambulizi ya anga kaskazini mashariki ya Syria

  (GMT+08:00) 2018-06-13 19:43:06

  Shirika la habari la Syria SANA limesema, watu 30 wameuawa katika mashambulizi ya anga yaliyofanywa na jeshi la muungano linaloongozwa na Marekani katika mkoa wa Al Hasakah, kaskazini mashariki mwa Syria.

  Jumatatu wiki hii, jeshi hilo lilifanya shambulizi la anga dhidi ya kambi ya wakimbizi wa Iraq mkoani Al Hasakah na kusababisha vifo vya watu 18, wakiwemo wanawake na watoto wengi, na siku inayofuata, jeshi hilo lilishambulia eneo la makazi la Tal Shayer, kusini mashariki mwa mkoa huo na kusababisha vifo vya watu 12.

  Habari zinasema, mashambulizi ya jeshi hilo yanaongezeka dhidi ya eneo la kusini la mkoa wa Al Hasakah na yanalenga kulidhibiti eneo hilo kwa kundi la wakurd la Syria linaloungwa mkono na Marekani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako