• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Russia kukutana na ofisa wa ngazi ya juu wa Korea Kaskazini

  (GMT+08:00) 2018-06-13 19:55:11

  Msemaji wa ikulu ya Russia Dmitry Peskov amesema, Rais Vladmir Putin wa nchi hiyo atakutana na rais wa bunge la Korea Kaskazini Bw. Kim Yong Nam hapo kesho mjini Moscow.

  Peskov amesema, Bw. Kim anakwenda Russia kuhudhuria ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Dunia ya FIFA, lakini hakutoa maelezo zaidi.

  Ziara ya Bw. Kim nchini Russia inakuja baada ya mkutano wa kihistoria kati ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un na rais Donald Trump wa Marekani uliofanyika nchini Singapore.

  Peskov amerejea tena nafasi ya Russia kuwa hakuna njia nyingine zaidi ya njia za kisiasa na kidiplomasia katika kutatua suala la Korea.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako