• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ongezeko la kasi la utoaji wa Cabon dioxide la China ladhibitiwa

  (GMT+08:00) 2018-06-13 20:40:45

  Leo ni Siku ya taifa ya upunguzaji wa utoaji wa hewa ya carbon dioxide nchini China, na kauli mbiu ya mwaka huu ni "kuinua uelewa wa mabadiliko ya hali ya hewa, kuimarisha nguvu za kutochafua mazingira".

  Naibu waziri wa mazingira wa China Bw. Zhuang Guotai amesema, katika miaka ya hivi karibuni, China imechukua hatua mbalimbali kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, na ongezeko la kasi la utoaji wa Cabon dioxide limedhibitiwa.

  Amesema China imechukua nafasi ya kwanza kwa nchi zinazotoa cabon dioxide kwa wingi, pia ni nchi inayoathiriwa vibaya na mabadiliko hali ya hewa. Katika miaka ya hivi karibini, China imechukua hatua mbalimbali kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kupata maendeleo makubwa. Mwaka jana utoaji wa cabon dioxide kila kuzalisha GDP fulani nchini China ulipungua kwa asilimia 46 kuliko mwaka 2005.

  Ameongeza kuwa, China itaendelea kuchukua hatua za kupunguza utoaji wa cabon dioxide, ili kutimiza lengo la utoaji wa hewa chafu kufikia kilele ifikapo mwaka 2030.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako