• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Fainali za kombe la dunia zinaanza leo kwa mechi kati ya Russia na Saudi Arabia

  (GMT+08:00) 2018-06-14 09:08:35

  Hatimaye siku imefika msikilizaji zimebaki saa chache kabla ya kuanza kwa mechi za fainali za kombe la dunia nchini Russia, sherehe za ufunguzi zitafanyika saa chache kabla ya mechi ya kwanza kuchezwa ikitarajiwa kutazamwa na mamilioni ya watu duniani. Kwenye nchi za Afrika Mashariki hali ya ajabu inatokea kwenye upande wa vituo vya televisheni kuoneysha michezo hiyo. Nchini Tanzania miungano kadhaa ya vituo vya televisheni imeanzishwa ili kuimarisha vikosi vya uchambuzi wa michezo hiyo, nchini Kenya nako NTV na kwese Sports wametangaza kuunda muungano utakaoonyesha mechi zote 32. Mashirika mengine kama vile Supersport wameamua kushusha gharama za ving'amuzi, na wengine kama kampuni ya starTimes ya hapa China imefikia hatua ya kualika wachambuzi kutoka Tanzania ili kufanya uchambuzi kwenye matangazo yao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako