• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kocha wa timu ya taifa ya Hispania afukuzwa siku moja kabla ya kombe la dunia kuanza

  (GMT+08:00) 2018-06-14 09:09:38

  Siku moja baada ya klabu ya Real Madrid kumtangaza kocha wa timu ya taifa ya Hispania Julen Loptegui kuchukua mikoba ya Zenedine Zidane kuifundisha klabu hiyo baada ya fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Russia, Chama cha soka Hispania kimefikia maamuzi ya kumtimua Julen Loptegui ukocha wa timu ya taifa baada ya kocha huyo kutangazwa kuwa atajiunga na Real Madrid, kitu ambacho hakijawafurahisha viongozi hao. Mkuu wa chama cha soka Hispania Luis Rubiales amekasirishwa na kitendo cha Julen kutangazwa mapema kuwa ataondoka Hispania, kipindi ambacho anaamini akili yake alipaswa kuiweka katika Kombe la Dunia na hakukuwa na ulazima wa kutangazwa mapema. Julen Loptegui anatimuliwa baada ya kuiongoza timu ya taifa ya Hispania katika michezo 20, ameshinda michezo 14, sare michezo sita, hakuna mchezo ambao amepoteza, timu imefunga magoli 61 na kuruhusu magoli 13 pekee. Nafasi yake inachukuliwa na kocha wake msaidizi Hirero.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako