• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kocha wa Simba arudi kwao Ufaransa baada ya kushindwa kusaini mkataba mpya

  (GMT+08:00) 2018-06-14 09:10:41

  KOCHA wa Simba, Pierre Lechantre ameaondoka jana nchini Tanzania na kurudi kwao Ufaransa baada ya kufikia makubaliano na uongozi wa Simba kuwa muda wake na klabu hiyo umefika mwisho. Mfaransa huyo aliisaidia Simba kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara baada ya kushindwa kufanya hivyo kwa miaka mitano. Alimaliza mkataba wake wa miezi sita wa kukinoa kikosi hicho na uongozi kushindwa kuingia makubaliano ya kumuongezea mkataba mpya. Msemaji wa Klabu ya Simba alisema siku chache kuwa siku za Leshante klabuli zilikuwa zinahesabhika

  Ingawa tarehe 18 bado haijafika Leshante tayari amepanda ndege na kurudi kwao. Na kabla ya kuondoka alisema kuna mambo muhimu ambayo wameshindwa kufikia makubaliano katika mkataba mpya, ndio maana ameamua kuondoka. Dalili za hatma yake zilianza kuonekana nchini Kenya ambako katika mechi ya nusu fainali ya kombe la Sports Pesa Super Cup hakuonekana kwenye benchi la Simba. Inaaminika kuwa ni uswahili ndio umefanya kocha huyo kuonekana hafai, wakati matokeo uwanjani yameonyesha kuwa ameleta mabadiliko na kuipatia ushindi wa ligi, na kufika nusu fainali ya kombe la sports pesa super cup.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako