• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki kuu ya Marekani yapandisha kiwango cha riba kwa mara ya pili mwaka huu

    (GMT+08:00) 2018-06-14 09:16:12

    Benki kuu ya Marekani imepandisha kiwango cha riba kwa asilimia 0.25, ikiwa ni mara ya pili kwa mwaka huu na mara ya saba tangu mwaka 2015. Taarifa iliyotolewa na benki hiyo imesema, kutokana na hali halisi na makadirio ya soko la ajira, na mfumuko wa bei, benki hiyo imeamua kupandisha kiwango cha riba hadi asilimia 2 kutoka asilimia 1.75. Kwenye ripoti mpya iliyotolewa jana, benki hiyo imekadiria kuwa uchumi wa Marekani utakua kwa asilimia 2.8 mwaka huu, na idadi ya watu wasio na ajira nchini Marekani itapungua na kufikia asilimia 3.6 mwishoni mwa mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako