• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda yaitaka mahakama ya kimataifa kutowaachia huru mapema waliofungwa kwa makosa ya mauaji ya halaiki

    (GMT+08:00) 2018-06-14 09:44:34

    Serikali ya Rwanda imeomba ofisi ya umoja wa mataifa inayoshughulikia mahakama za kimataifa (MICT) iliyoko mjini Arusha, kuzuia kuachiwa mapema kwa watu watatu waliohukumiwa kifungo na mahakama ya makosa ya jinai kuhusu Rwanda.

    Nakala ya ombi la serikali ya Rwanda inaonyesha kuwa serikali imemwomba ofisa wa ofisi hiyo jaji Theodor Meron, azuie kuachiwa huru kwa wafungwa Aloys Simba, Dominique Ntawulilyayo na Hassan Ngeze. Ombi la watatu hawa kuachiwa mapema lilitolewa Mei 22.

    Kwenye ombi lake, serikali ya Rwanda imesema watu hao walifanya uhalifu ambao unakiuka vigezo vyote vya ubinadamu, maadili na utu dhidi ya mamilioni ya watu. Na hawajawahi kujutia makosa yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako