• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yasema mkutano wa Kim na Trump ni mwanzo mzuri

  (GMT+08:00) 2018-06-14 09:58:42

  Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema mkutano kati ya viongozi wa Korea Kaskazini na Marekani una umuhimu mkubwa wa kihistoria.

  Bw. Geng Shuang amesema mkutano huo umekuwa na matokeo mazuri ambayo ni maendeleo muhimu katika kuhimiza mchakato wa kuondoa silaha za nyuklia kwenye Peninsula ya Korea, na kuleta ufumbuzi wa kisiasa wa suala hilo.

  Rais Donald Trump wa Marekani amesema Korea Kaskazini haitakuwa tena tishio la nyuklia, tatizo kubwa na la hatari kwa Marekani, na pia anatarajia Korea Kaskazini itakuwa na mustakabali mzuri katika siku za baadaye.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako