• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema Afrika ni mwenzi muhimu katika Pendekezo la "Ukanda moja, Njia moja"

    (GMT+08:00) 2018-06-14 09:59:10

    Balozi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Ma Zhaoxu, amesema Afrika ni mwenzi muhimu katika maendeleo ya pendekezo la "Ukanda mmoja, Njia moja".

    Bw. Ma Zhaoxu amesema pendekezo hilo linakidhi mahitaji ya Afrika na kutafuta faida za kunufaisha pande zote mbili, na litatoa msaada kwa Afrika kwenye msingi wa kuiheshimu na kuimarisha urafiki.

    Pendekezo la "Ukanda mmoja, Njia moja" linahusisha zaidi ya nchi 20 barani Afrika. Makubaliano ya ushirikiano yanahusisha miradi 39 katika sekta 17 zikiwemo reli, barabara kuu, bandari na nishati.

    Mwenyekiti wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Bw. Miroslav Lajcak amesema, pendekezo la "Ukanda mmoja, Njia moja" ni hatua ya China kutekeleza ahadi yake katika Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa SDGs na utaratibu wa pande nyingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako